Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:32 am

NEWS: KANISA KATOLIKI CONGO LIMESEMA BADO LINAMJUA ALIYESHINDA UCHAGUZI

Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Cenco) limesema kuwa linafahamu jina la mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Desemba 30 nchini DRC na kuomba Tume ya Uchaguzi (CENI) kutangaza matokeo katika hali ya "ukweli na haki ".

Baraza hilo limesema lina sampoli ya wawakilishi iliyochapishwa katika vituo vya kupigia kura ambavyo vinawauhusu kujuwa jina la rais aliechaguliwa. Sampuli hiyo ni ya vituo zaidi ya elfu 23 kati ya vituo elfu 70 vilivyowekwa na Ceni.

Tume ya uchaguzi ilitarajiwa kutangaza matokeo Jumapili ya kesho lakini kunataarifa kuwa huenda ikachelewa kufanya hivyo kwani bado haijapokea matokeo kutoka vituo vingi vya kupigia kura nchini humo.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) Corneille Nangaa alisema matokeo ya zaidi ya asilimia 80 ya kura bado yanasubiriwa.

Upinzani pia umelalamikia dosari kwenye uchaguzi huo.

Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 17 na ameahidi kukabidhi madaraka kwa atakayeshinda uchaguzi.

kwamujibu wa msemaji wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC Donatien Nshole, amesema sio jukumu lao kutangaza matokeo wao ni waangalizi lakini wanafahamu nani aliechaguliwa na wananchi.

"Ni muhimu kusisitiza kuwa kasoro zilizojitokeza haziwezi kuathiri kwa kiwango kikubwa chaguo la wananchi wa DRC walioonyesha wazi katika uchaguzi wa urais wa Desemba 30," msemaji wa Cenco ameongeza."

Cenco imeitaka Tume ya Uchaguzi (CENI) kama taasisi inayounga mkono demokrasia kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa heshima ya ukweli na haki," amesema Padri Nshole.

Msemaji wa Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC (Cenco) amekuwa anawasilisha ripoti ya awali ya ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi wa Tume ya Haki na Amani ya Cenco, ambayo inasema kuwa ilikuwa na waangalizi 40,000 wakati wa uchaguzi wa siku ya Jumapili.

Uchaguzi Mkuu wa Jumapili utapelekea kumpata mrithi wa Rais Joseph Kabila, ambaye hakuruhusiwa kuwania muhula wa tatu kulingana na Katiba.

Siku ya Jumanne CENI ilisema kuwa itatangaza matokeo ya awali siku ya Jumapili Januari 6, 2019. Siku ay Alhamisi CENI ilisema kuwa kuna uwezekano zoezi hilo liahirishwe.

Raia nchini DRC bado wanasubiri kutangazwa matokeoa ya uchaguzi huo.

hali ya wasiwasi bado inaendelea, huku huduma ya intaneti ikiendelea kufungwa na mitambo ya radio ya kimataifa RFI ikizimwa.

Wakati huo huo Tume ya Uchaguzi CENI imesema kuwa tayari imehesabu asilimia 20 tu ya kura zilizopigwa.