- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAMATI KUU CHADEMA YAMUHOJI SAED KUBENEA
Dar es Salaam: Kamati Kuu ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema kimefanya kikao leo Octoba 17, 2018 kwa lengo la kuwahoji wabuge wawili wa chama hicho Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea na mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu.
Chama kilianza kumuhoji Komu na baadae kikaanza kumuhoji Mbunge Saed Kubenea
Kikao hicho kinachofanyika katika ukumbi wa Ledger Plaza katika Hoteli ya Bahari Beach kinajadili masuala mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya chama hicho likiwamo la wabunge hao.
Kubenea na Komu katika siku za hivi karibuni wamezua mjadala ndani na nje ya chama hicho kwa kile kinachodaiwa ni sauti yao inayosikika wakipanga mpango hasi dhidi ya Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.
Wabunge hao kwa nyakati tofauti wamekana kuhusika na sauti hiyo kwa kile walichoeleza ni ya kutengeneza huku Jacob ambaye ni Diwani wa Ubungo (Chadema) naye akieleza kupeleka suala hilo ndani ya chama.
Komu ametoka katika kikao hicho saa 11:32 jioni na alipotakiwa na waandishi kueleza nini alichohojiwa amesema hana mamlaka ya kuzungumzia chochote.
“Kwa mujibu wa katiba ya chama changu sina mamlaka ya kuzungumza chochote suala hilo lipo ndani ya kikao,” amesema Komu.
Wabunge hao leo saa 8:01 mchana walionekana nje ya ukumbi huo wakisubiri maelekezo ya kuingia katika kikao hicho.