Kamanda Shana amebainisha kuwa Askari Polisi hao wamekutwa na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya uuzaji wa nyara za serikali aina ya meno ya tembo kitu ambacho ni kinyume na maadili ya jeshi.
Amewataja askari hao kuwa ni H. 5461 PC Enock wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoa wa Mwanza na H. 4165 PC Robert wa kikosi maalum, ambao walikutwa na vipande viwili vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 20 katika eneo la Nyamhongolo Ilemela Mwanza.
Aidha kamanda amesema Jeshi la Polisi mkoani humo, linaendelea na operesheni maalum kuwasaka waliokuwa wakishirikiana na askari katika biashara hiyo.
Askari polisi waliofukuzwa kazi wanashikiliwa na watafikishwa mahakani siku ya ijumaa Agosti 31, 2018 kwaajili ya kufunguliwa mashtaka