- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAMANDA MROTO AAHIDI KUMKANGUA KIONGOZI YEYOTE SEREKALINI
Dodoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema anapofanya ukaguzi wa magari barabarani akibaini aliyefanya kosa atamkamata hata akiwa kiongozi mkubwa serikalini.
Muroto ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 20, 2018 alipotembelewa na waandishi wa habari walio katika mradi wa usalama barabarani unaosimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, kikosi cha usalama barabarani na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Muroto ambaye aliongozana na jopo hilo hadi eneo la Kisasa jijini hapo, amesema changamoto ilikuwa namna ya kubadilisha mtazamo wa madereva wengi hasa wa Serikali.
“Muda mwingi nipo barabarani nakamata viongozi wakubwa na hata bodaboda ili mradi amefanya kosa siangalii usoni, huko kote Chamwino, mimi siangalii huyu kiongozi au mtu wa kawaida ilimradi amevunja sheria lazima awajibishwe,” amesema.
Hata hivyo, Muroto amesema ajali nyingi husababishwa na waenda kwa miguu, madereva, abiria na wengi bado wanahitaji elimu ili kuondoa ajali za barabarani.