Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:05 pm

NEWS: KAMANDA KIOMBWE : ''JELA MIEZI 6 KWA MATUMIZI MABAYA YA NAMBA YA DHARULA'

DODOMA: Kamanda kikosi cha Jeshi la zimamoto Mkoa wa Dodoma Regina Kiombwe amesema hatua kali zitachukuliwa kwa wale wote watakao tumia namba ya dharula ya jeshi hilo 114 kinyume na matumizi yake watafungwa kifungo cha miezi sita jela.

Kauli hiyo imetolewaleo kwenye uzinduzi wa namba 114 itakayotumika kwa wananchi kuita jeshi la zimamoto na uokoaji pindi wanapopata majanga ya moto.

Kiombwe amesema kuwa wananchi wasitumie namba hiyo kinyume na matumizi yake namba 114 nikwaajili majangga ya moto na sio kwa mzaha au kwamatusi.

“ Tumetoa namaba hii kwa makusudi husika kwani baadhi ya wananchi wamekuwa wakija ofisni na kutoa taalifa juu ya janga la moto badala ya kupiga simu na tuwafuate mahala husika hivyo naamini namaba hii itawasaidia wananchi kupiga simu huko huko sehemu ya janga la moto lilipotokea,”amesema Kamanda Kiobwe.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dodoma Jodan Lugimbana amesema kuwa moja ya huduma inayotakiwa kwa muda huu ni huduma sahihi ya upatikanaji wa namba ya uokoaji wa jeshi la zima moto.

Amesema jamii inapaswa kujiandaa na majanga ya moto kwa kujifunza elimu juu ya kuzuia majanga hayo na hivyo jeshi la zimamoto limeonyesha njia ya namna gani wananchi wanaweza kupata msaada pindi wanapaunguliwa na nyumba zao.

Aidha amelitaka jeshi hilo kuhakikishawanatoa elimu kwa wananchi kwani kwakufanya hivyo wataweza kuzuia majanga hayo ya moto .

“ Nasema hivyo kwamaana nimepata taarifa majanga mengi ya moto yanayotokea nimajanga yanayoweza kuepukika hivyo ningependa namba hii esambae kote na hata katika wilaya zote za mji huu,”amesema Lungimbana.