- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: KAMA UTAPOTEZA PASSPORT YAKO ITAKUGHARIMU SH. 500,000 KUPATA MPYA
Dar es Salam: Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imesema Mtu yeyote atakayepoteza hati ya kielekroniki ya kusafiria ambayo kwa sasa inapatikana kwa Sh150,000 itamlazimu kugharamia kulipa Sh500,000 kupata mpya. Aidha, kama ataipoteza mara ya pili itamgharimu Sh750,000 ili aweze kupata nyingine.
Mpaka kufikia sasa tayari hatai za kusafiria 15,101 zimeshatolewa kwa watanzania tangua walipoanza mfumo huo wa hati za kieletroniki mwezi Januari mwaka huu
Akiongea Jana May 25 Kamishna wa Uhamiaji, Uraia na Pasipoti, Gerald Kihinga katika uzinduzi wa utoaji wa hati hizo Dar es Salaam alisema kuwa gharama hiyo itasaidia watu kutunza hati zao.
Alisema zipo kesi nyingi za watu kupoteza hati zao za kusafiria na baadhi yake ni zile zinazotokea katika matukio yasiyohitaji uwapo wake. “Utakuta mtu anakuja kuomba hati mpya, ukimuuliza mazingira (ilivyopotea) anasema alikuwa akielekea Kariakoo kutoka Buguruni, sasa huko Kariakoo hati hiyo unaenda nayo ya nini? Tuzitunze hati hizi kwa sababu ni nyaraka muhimu kwa nchi yetu,” alisema Kihinga.
Alifafanua kuwa hakuna haja ya kuzunguka na hati hiyo kila mahali isipokuwa yale maeneo muhimu yanayohitaji uwapo wake kuepuka gharama kubwa ya upatikanaji wake wakati inapopotea. Pia, alieleza kuwa tangu kuanza kutolewa kwa hati hizo hakuna changamoto zilizojitokeza zaidi ya kuwapo baadhi ya watu wanaotumia mawakala kupata hati na hivyo kutozwa zaidi ya Sh300,000. “Niwasihi tu wasitumie mawakala hawa, waende wao wenyewe kupata huduma hii, inatolewa kwa muda mfupi ikilinganishwa na hapo zamani hakuna usumbufu na kuwatumia mawakala,” alisema.
Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Chrispin Ngonyani alisema upo udhibiti wa kutosha kuhakikisha kila anayeomba hati hiyo anapewa kwa wakati bila bugudha wala usumbufu wowote. Awali, akizindua hati hizo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema badala ya kulipa gharama kubwa kupata hati hiyo baada ya kuipoteza ni vizuri Watanzania kujenga tabia ya kuzitunza zidumu kwa muda mrefu