Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:32 am

NEWS: KAFULILA AJIVUA UWANACHAMA CHADEMA

Dar es salaam: Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini NCCR Mageuzi (2010-2015) David Kafulila amejivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kutokuwa na imani tena na upinzani katika kupambana na ufisadi.

Kafulila amesema kuwa bado anatafakari atakwenda kwenye jukwaa lipi la siasa ili kuendeleza harakati zake dhidi ya ufisadi.
Sababu nyingine aliyoitaja kumuondoa Chadema ni upinzani kukosa ajenda ya ufisadi kutokana na Rais John Magufuli kuibeba ajenda hiyo kwa vitendo hasa baada ya watuhumiwa na wahusika wa rushwa kubwa kubwa kufikishwa mahakamani,

Hivi karibuni matokeo ya tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na mashirika huru ya ndani na nje ya nchi yanaonyesha kiwango cha rushwa nchini kimeporomoka.
“Nikiwa mmoja wa wanasiasa vijana nilibahatika kutumikia Bunge la 10, siku zote nimejipambanua na kujitoa mhanga kupambana na ufisadi kupitia jukwaa la bunge, vyama vya siasa na shughuli mbalimbali za kijamii kwa ujumla.

“Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni na hasa tangu harakati za uchaguzi mwaka 2015 vyama vya upinzani nchini vibnaonekana kuoigwa ganzi na kupooza katika juhudi zake za kuopambana na ufisadi, ghafla ufisadi siyo tena ajenda kuu ya upinznai nchini kwa sababu ni wazi kuwa upinzani siyo tena jukwaa la kuendesha vita dhidi ya ufisadi,” amesema Kafulila katika taarifa yake.