Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:49 pm

NEWS: JUMLA YA WANAWAKE 556 HUPOTEZA MAISHA KWA VIFO VYA UZAZI.


DODOMA: Imeelezwa kuwa jumla ya wanawake 556 kwa mwaka 2015/16 kwa kila vizazi hai laki moja hupoteza Maisha kutokana na vifo vitokanavyo na uzazi ambapo takwimu zinaonyesha kwa mwaka 2010 vifo hivyo vilipungua hadi kufikia 454.

Hayo yamesemwa na mkurungezi idara ya uuguzi na ukunga nchini Dr Gustan Moyo kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya afya, wakati akifungua mkutano Wa uchehchemuzi (ADVOCACY) ya ajira kwa wauguzi na wakunga kwa kanda ya ziwa na kanda ya Magharibi ulifanyika Leo mjini hapa.

Dr Moyo amesema takwimu za kuhusu watumishi Wa afya kwa mwaka (2012/2013) zinaonyesha kuwa ni asilimia 55 ya wafanyakazi Wa afya ndio wanaotoa huduma vijijini na maeneo yasiyofikiwa kiurahisi ambao kuna zaidi ya asilimia 75 ya watanzania.

Hata hivyo amesema ili kukabiliana na tatizo la upungufu Wa wauguzi na wakunga wizara ya ya afya kwa kushirikiana na mradiwa more and better midwives for rural Tanzania wamejipanga Kuelimisha jamii na wanafunzi Wa sekondari juu ya kuitambua fani ya uuguzi pamoja na mchango wake katika huduma ya afya ya uzazi ya mama na mtoto, na kushawishi vijana wanaohitimu Elimu ya sekondari kusomea gani ya uuguzi na ukunga.

Pia kuviwezesha vyuo vya uuguzi na ukunga ili kutoa wauguzi wakunga wenye weledi na ujuzi stahiki katika utoaji Wa huduma mbalimbali za afya hasa za mama na mtoto.

Aidha ameongeza kuwa serikali imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo hivi karibu ilitoa ajira 3000 katika kuongeza idadi ya watumishi lakini pamoja na hayo amesema upungufu Wa Wa wafanyakazi Wa afya hususani wauguzi na wakunga.

Naye mwakilishi wa Amref Dr Aisa Nkya Muya Amesema ili kutatua tatizo hilo shirikiano ni muhimu kwa wadau na serikali kuungana na kupeana mawazo jinsi yakufanya ili kukabiliana na suala hilo.

Mradi huo ni Wa miaka mitano tokea mwaka (2016_2021 lengo ku u la mradi huo nikuboresha afya na ustawi Wa akina mama na watoto.