- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JUMLA YA WANAFUNZI 650,862 WACHANGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA.
DODOMA: Jumla ya wanafunzi 650,862 sawa na asilimia 98.31 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza kwa mwaka 2018 kati ya wanafunzi 662,035 waliofaulu.
Pia imeelezwa kuwa mwanafunzi atakayechelewa kuripoti wiki mbili baada ya shule kufunguliwa nafasiyake atapewa mwanafunzi mwingine.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Selemani Jafo alisema ufaulu huo ni sawa na ongezeko la wanafunzi 124,209 ambapo ni sawa na asilimia 23.58.
Amesema katika kindi cha mwaka huu wanafunzi 1,912 wenye mahitaji maalum waliofaulu mitihani ya darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.
Aidha Jafo amesema kuwa wanafunzi 11,173 sawa na asilimia 1.69 ya waliofauru hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu hiyo ya kwanza ya uchaguzi.
“Sababu iliyopelekea wanafunzi hao kutokuchaguliwa imetokana na uhaba wa miundombinu ya elimu ikiwemo vyumba za madarasa kwenye baadhi ya halmashauri”amesema Jafo.
Akitaja mikoa ambayo halmashauri zake zimeshindwa kuchagua wanafunzi alisema ni Lindi wanafunzi 170, Mbeya (3,092), Rukwa (4,091), Manyara (1,268), Katavi (976), na Simiyu ( 1,576).
“ Halmashauri ambazo zimeshindwa kuwapangia wanafunzi wote waliofaulu nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 katika awamu ya kwanza ni pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wanafunzi 170”amesema Jafo.
Halmashauri zingine ni wilaya ya Chunya wanafunzi 80, Halmashauri ya wilaya ya Mbeya wanafunzi 207, Halmashauri ya Jiji la Mbeya wanafunzi 1,227, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali 1,578.
Zingine ni Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo wanafunzi (166), Nkasi wanafunzi (1,318),Halmashuri ya Wilaya ya Sumbawanga wanafunzi (1,054),Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wanafunzi (1,553). Halmashauri ya Babati (581), na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang wanafunzi 687.
Ametaja Halmashauri zingine ni Mpanda (262), Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo (714), Halmashauri ya Mji wa Bariadi (369), na Halamshauri ya Wilaya ya Busega wanafunzi 1,207.
Wakati huohuo waziri Jafo ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa aliyoitaja kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wote wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018.
“Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani wanatakiwa kuripoti shuleni tarehe 18 January 2018”amesema Jafo.
Pia amesema mikoa ambayo inatatizo la miundombinu ni lazima ikamilishe miundombinu hiyo haraka ili wanafunzi watakaochaguliwa awamu ya pili waweze kuripoti shuleni kabla ya tarehe 15 Februari 2018.
Hata hivyo Jafo amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kutumia fursa hiyo vizuri katika kujifunza na kuachana na anasa au starehe amabazo zitawafanya kupata matokeo mabaya ya kuhitimu kidato cha nne.