- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JUMLA YA WAGONJWA 35 HUTIBIWA NJE YA NCHI KILA MWAKA
DODOMA: Naibu waziri wa Afya ,maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali imekuwa ikipeleka wastani ya wagonjwa (35)kwa kila mwaka nje ya Nchi ikiwemo India kwa ajili ya kupandikiza figo.
Ameyasema hayo leo kwa niaba ya waziri Ummy Mwalimu wakati akifungua mkutano wan ne wa chama cha madaktari wataalamu wa figo Tanzania ambao umefanyika mjini hapa.
‘’ Wagonjwa ambao waliokwisha kupandikizwa figo na ambao wanafatilia matibabu yao katika Hospital ya Taifa muhimbili ni taktibani 204,’’amesema. .
Akifafanua zaidi Ndugulile ameeleza gharama za kupandikiza figo nje ya Nchi ni wastani wa fedha za kitanzania sh milioni 75 hadi 77 (tsh75,000.00- 77,000.00) kwa mtu mmoja hii,ikijumuisha upandikizaji wa figo ,nauli na malazi.
Amesema kwa kufanya hivyo upandikizaji wa figo hapa Nchini ,bajeti ya mgonjwa mmoja itakuwa milioni 20.3 na hiyo inamaanisha kwamba,kwa bajeti ya kupeleka mgonjwa mmoja nje kwaajili ya kupandikiza figo ,na kwa sasa wanaweza kuwapatia huduma hiyo wagonjwa wa 3 hadi 4 hapa Nchini na huduma hizo zikianza kutolewa hapa nchini zitaipunguzia mzigo serikali na watanzania lakini pia wataweza kuwafikia wagonjwa wengi zaidi.
Ameongeza kuwa idadi ya wagonjwa walio kwenye hatua za mwisho za ugonjwa wa figo ambao wanahitaji upandikizaji wa figo imekuwa ikiongezeka kila mwaka .pia kwa mwaka 2011-2012 wagonjwa waliokuwa wanafanyiwa huduma ya kusafisha damu kutokana na figo kushindwa kufanya kazi ,walihudumiwa na mfuko waTaifa wa Bima ya Afya (NHIF) walikuwa mia moja na sabini na nane (178) .
‘’Kwa sasa wagonjwa 783 waliokuwa wanachama NHIF wameshafanyiwa usafishaji wa damu ili kutoa sumu kutokana na figo kushindwa kufanya kazi.’’amesema
Kwa upande wake daktari bingwa kutoka hospital ya Benjamini mkapa UDOM dk Alfred Jackson alisema wao wapo katika maandalizi ya upandikizaji wa figo hapa Tanzania na jitiada zinaendelea muhimbili na ikiwezekana ndani mwezi ujao mwanzoni wataweza kufanya huduma ya kwanza ya upandikizajio wa figo hapa nchini.