Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:53 pm

NEWS: JUKWAA LA WAKULIMA DOM LAIOMBA SERIKALI SEKTA YA KILIMO KUPEWA KIPAUMBELE.

DODOMA: Jukwaa la wakulima wadogowadogo mkoani Dodoma limesema ili Tanzania kufikia asilimia 10 kwenye sekta ya kilimo ni lazima serikali iwe kipaumbele kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo.



Hayo yamesema na Menyekiti wajukwaa la wakulima wanawake Chamwino(JUWACHA) Janeth Nyamayahasi wakati wa mkutano wakutoa taarifa ya pima kadi (huduma za Umma)katika wilaya ya chamwimo uliofanyika mjini hapa.

Amesema ili Tanzania kuweza kuboresha sekta ya kilimo ni lazima serikali kutatua changamoto ikiwemo ukosefu wa pembejeo kwa wakulima, kutoa elimu kwa wanawake ili kuwajengea uwezo wa kumiliki ardhi.

‘’Sisi kama wakulima wadowadogo ni lazima tupambane ili kupunguza changamoto kwa wakulima na taifa kiujumla ili tusonge mbele’’,amesema.

Nyamayahasi amesema vikwanzo vingine ni uhaba wa fedha, ukosefu wa miundombinu ya kutosha na riba kubwa zinazotozwa na benki kwenye mikopo.

Mbali na hayo ameiomba serikali kupitia benki ya wakulima ifikishe huduma kwa kila mkoa ili kutatua changamoto hizo.

‘’Benki iweke kipengele kinachotambua hati za kimila au zinazotolewa kupitia mpango wa matumizi bora ya ardhi,’’amesema.

Aidha alisema ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo ni kuendelea kuijengea uwezo jamii ili kuweza kuboresha kilimo.

‘’vikundi vya wakulima vya wakulima kwa kusaidiana na viongozi kuhakikisha ushiriki wa wananchi kwenye mikutano ya kijamii,’’amesema.

Moja ya washiriki hao Martha Keneth alisema ni lazima jamii kupata elimu juu ya kupanda mti kukata mti ili kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

‘’kiwango cha mavuno kwa eneo kimekuwa kikivupungua , kufautia uwepo wa mtawanyiko mbaya wa mvua ikiwemo mvua kuzidi , ukame na joto liliptiliza,’’amesema.

Naye Mratibu wa mradi wa PFA unawezesha umma kifedha katika kilimo unaofadhiriwa na shirika la Action Aid Joram Wimmo amewataka wakulima hao kuwekeza na kushirikiana na halmashauri zote katika sekta ya kilimo ili kukuza kilimo nchini .

’’kwa sababu Tanzania yetu itajengwa na sisi wenyewe na kama tunataka kuibomoa basi tutaibomoa wenyewe,’’amesema.

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Sophia Swai amesema ili kufikia lengo ni lazima kufanyakazi kwa ushirikiano na kuongeza kuwa changamoto kubwa katika idara yake ni ukosefu wa mapato ndani ya halmashauri na vikundi vingi kutokuwa waamini.

‘’lazima nikiri tuna miaka mitano hatujatoa hela ni kutokana na pato la halimashaurikuwa hafifu;’’amesema.

‘’Mpaka sasa tumetenga sh milion 10 kwaajili ya wakinamama na vijana lakini vikundi vingi ni hewa,’’amesema.

Kwa mujibu wa Tamwimu za ukuaji wa sekta ya kilimo kwa mwaka 2016/17 kilimo kimeonekana kupungua kwa asilimia 1.7 tofauti naasilimia 3.5 kwa mwaka 2011.