- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JIJI LA TANGA LAPONGEZWA KWA MIRADI BORA.
TANGA: Halmashauri ya Jiji la Tanga imepongezwa kwa kujenga miradi ya maendeleo yenye viwango vinavyoridhisha.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo alipokuwa katika ziarani ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Tamisemi mkoani Tanga.
Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ametembelea ujenzi wa Dampo la kisasa linalojengwa kwa Sh.Bilioni 9, uboreshaji wa kituo cha afya cha Mikanjuni kinacho gharimu sh.Milioni 400 pamoja kiwanda cha kufyatua matofali cha halmashauri ya Jiji kilichogharimu Sh.milioni 80.
Katika ukaguzi wa miradi hiyo, Waziri Jafo hakuacha kumsifu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi inayojengwa kwa ubora mkubwa.
Aidha, Waziri Jafo amemmwagia sifa Mkurugenzi huyo kwa ubunifu mkubwa wa kuanzisha kiwanda cha kisasa cha matofali kinachotumia teknolojia ya kisasa zaidi ambacho kinauwezo wa kufyatua matofali zaidi ya 5000 kwa siku ambapo hadi sasa wameshapata tenda ya kutengeneza matofali 100,000 kutoka kwa kampuni moja pekee huku makampuni mengine na wananchi wa kawaida wakimiminika kiwandani hapo kutaka matofali kutokana na ubora mkubwa wa matofali hayo.
Waziri Jafo amewataka wakurugenzi wa halmashauri nyingine hapa nchini kuiga mfano huo mzuri wa vyanzo vya mapato ili kuziongezea mapato halmashauri zao.