Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 6:32 am

NEWS: JESHI LA ZIMBABWE LIMECHUKUA UDHIBITI RASMI NCHI NZIMA

HARARE: Jeshi la Zimbabwe limedhibiti maeneo kadhaa muhimu pamoja na majengo ya serikali. Baadhi ya mawaziri wamewekwa chini ya ulinzi.

Mpaka sasa Rais wa Zimbabwe Bw. Robert Mugabe amewekwa chini ya kifungo cha nyumbani na mkewe Grace Mugabe, ambaye ni mmoja wa wahusika wakuu wa mgogoro huo wa kisasia, anaripotiwa kutorokea nchini Namibia. Hata hivyo jeshi bado linakataa kuzungumzia iwapo ni mapinduzi ya kijeshi yanayoendelea au Laa.

Mataifa mengi na Jumuiya za kimataifa zimetoa wito kwa pande zote mbili kujizuia na kurejea kwa hali ya utulivu nchini Zimbabwe ili wasisababishe nchi kuingia kwenye machafuko.

Uingereza kupitia waziri wake wa Mambo ya Nje Boris Johnson, imeonya kuhusu "serikali ya mpito ambayo itaongozwa na mtu ambaye hakuchaguliwa na raia".

"Tunaangalia kwa makini hali inayoendelea nchini Zimbabwe. Hali bado ni tate, "Waziri Mkuu Theresa May aliwaambia Wabunge wa Uingereza kabla ya kutoa wito " kwa pande zote kujizuia na machafuko".


Siku ya Jumatano mchana Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, mshirika wa karibu wa Robert Mugabe aliongea kwa simu mkongwe huyo wa uhuru wa Zimbabwe na alihakikisha kwamba yuko chini ya kifungo cha nyumbani.

Jacob Zuma, ambaye alisema "ana wasiwasi" ana hali inayoendelea Zimbabwe, aliwatuma mawaziri wake wawili mjini Harare kwa niaba ya Jumuiya ya nchi za kusini mwa ukanda wa Afrika (SADC) anayoongoza. Wajumbe hawa wawili wa rais wa Afrika Kusini wawasili Harare. Wanatazamiwa kukutana na kiongozi wa zamani wa uhuru na viongozi wa jeshi, wakisubiri mkutano utakaofanyika Alhamisi alasiri mjini Gaborone.