- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI LAZUIA MKUTANO WA MBUNGE PETER MSIGWA
Iringa: Jeshi Polisi Mkoani Iringa limeuzuia Mkotano wa Hadhara wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa katika viwanja vya Mwembetogwa mjini hapo kwasababu za kiusalama na kwamba hakuna Polisi wa Kutosha mkoani hapo wa kusimamia Mkutano huo, kwa madai ya kwamba Askari wengi wapo kwenye shughuli za kitaifa.
Taarifa kutoka Ofisi ya Chadema Iringa Leo Novemba 24, 2018 kupitia katibu wa Chadema Mkoa hapo Bw. Jackson Mnyawami amesema walitarijia kufanya mkutano huo leo, lakini wamepokea barua ya polisi ikiwataka wasiendelee na mkutano huo hadi siku nyingine.
Barua ya Novemba 21, 2018 iliyotolewa na mkuu wa polisi Wilaya ya Iringa kwenda kwa mbunge huyo inaeleza kuwa mkutano huo umezuiwa kutokana na taarifa za kiintelejensia.
“Polisi Iringa tunazo taarifa kuna kikundi cha watu wanaojiandaa kufanya fujo katika mkutano huo. Hali hiyo inaweza kuleta uvunjifu mkubwa wa amani,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.
“Hakuna askari wa kutosha kwa ajili ya kusimamia mkutano huo kwani nguvu kazi kubwa imeelekezwa katika shughuli maalum za kitaifa ya usimamizi wa mitihani ya kidato cha nne, cha pili na darasa la nne.”
Mnyawani amesema wameipokea barua hiyo ya polisi ikiwa na sababu mbalimbali.
“Sababu tulizoelezwa ni za kiintelejensia kwamba kuna watu watafanya vurugu lakini pia wamesema kuwa kuna shughuli za kitaifa, ikiwa ni pamoja na mitihani inayoendelea kufanywa na wanafunzi wa kidato cha nne,” amesema.