- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI LAWAUWA MAJAMBAZI 6 DAR ES SALAAM
Dar es salaam: Jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kuwauwa majambazi 6 na kukamata bunduki aina ya AK47 tatu, risasi 217 mabomu ya kivita 8, na magazini 8 katika eneo la Ubungo jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari leo Novemba 29, 2018 Kamanda wa Polisi Kanda maalum Lazaro Mambosasa amesema Majambazi hao waliuawa baada ya mtego wa Polisi baada ya kupataa taarifa ya kuvamia bank za hapa mjini katikatika.
"Tulipata taarifa kuna majambazi wengine.
Willey Ilakozes, Omary Nassor(Mtanzania) ndio Walipanga kumvamia mwanabiashara.
Kuna gari tulikuta lilikuwa na Sh. Mil 50 maeneo ya Mabibo. Tegeta walivamia mchina na kumpora Sh. mil 10.
Huyu Irakoze ni Komando. Alishaua Polisi wawili, Kahama walishawahi kuua askari 2 na kutoroka na AK 47 MBILI"
Mwaka 2012 Irakoze alishawahi kuvamia mgodi na maduka ya Zanzibar" alisema Kamanda Mambosasa.
Aidha aliongezea kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vizuri. Watanzania wanaotegemea kupata kipato kwa kuvunja sheria, wataishia mikononi mwa Polisi. Ni wakati wa kubadilika, wenye kufanya matendo hayo hawatabaki salama.
"Yeyote atakayejaribu kupambana na jeshi la Polisi, hatabaki salama"