Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:42 am

NEWS: JESHI LA POLISI LAWAMANI KWA KUWAFUMBIA MACHO WATUMIWA WANAWAPA MIMBA WANAFUNZI.

DODOMA: Jeshi la polisi wilayani Bahi Mkoani Dodoma limelalamikiwa kuwafumbia macho watuhumiwa wanaowapa mimba wanafunzi sambamba na kuleta uchonganishi baina ya viongozi kutokana na kuwarudishia kesi za watuhumiwa wa mimba wanazokwenda kuziripoti.

Malalamiko hayo yametolewa hii leo na diwani wa kata ya Ibugule, Blandina Magawa katika kikao cha wadau wa elimu wilaya ya bahi ambapo amesema moja ya kesi ambayo haijatendewa haki ni ya kukamatwa kwa mtuhumiwa aliyempa mimba mtoto wa darasa la tano kufikishwa mahakamani na kuachiwa huru na badala yake kesi hiyo kupewa mtendaji wa eneo hilo aliyekuwa akipeleka ushahidi.

Fufuatia kitendo hicho Magawa amesema inawezekana suala hilo pia limegubikwa na vitendo vya rushwa hivyo kuiomba Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU ) kuingilia kati sakata hilo ili haki iweze kupatikana.

Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa kituo cha polisi wilayani Bahi,Mratibu Msaidizi wa polisi (asp) Fulgence Alfredy amesema viongozi wanapaswa kufatilia kesi hizo hadi ngazi ya mwisho huku akiongeza kuwa kesi ikishafika mahakamani anayehusika ni hakimu na si polisi.

Aidha naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo ya bahi Elizabeth Simon amekiri kuwa akipokea malamiko hayo kwa wingi huku akisema kesi nyingi zimekuwa zikiishia polisi na hazifiki mahakamani na kuwa kumekuwa changamoto ya kukatishwa tamaa kwa watoa ushahidi