Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:30 am

NEWS: JESHI LA POLISI LAMUHOJI JANUARY MAKAMBA SAKATA LA MODEWJI

Dar es Salaam: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam jana usiku Oktoba 21, 2018 linadai kufanya nae mahojiano kwa saa kadhaa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba kuhusiana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’.

Akizungumza na muakilishi.com baada ya kupata tetesi leo Jumatatu Oktoba 22, 2018 Kamanda wa Polisi wa kanda Maalum, Lazaro Mambosasa amekiri kumfanyia mahojiano Waziri Makamba lakini waziri huyo aliruhusiwa jana hiyo jiyo kuondoka baada ya kuhojiwa.

“Eeeennh Ni kweli tumemhoji Waziri Makamba jana usiku na kumwachia. Tumemhoji kuhusu suala la Mo Dewji,” ila kama kunahaja ya kutoa taatifa zingine tutawaeleza amesema Kamanda Mambosasa.

Sasa kama Utakumbuka Waziri Makamba ni miongoni mwa watu waliopata taarifa mapema sana za kupatikana kwa bilionea huyo na kuandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

“Mohammed Dewji amerudi nyumbani salama. Nimezungumza naye kwa simu dakika 30 zilizopita. Sauti yake inaonyesha mzima bukheri wa afya. Shukrani kwa wote kwa dua na sala. Naenda nyumbani kwake kumuona muda huu.”

Kitendo hicho kiliibua maswali mengi mitandaoni, watu wa kada mbalimbali wakihoji nani alianza kuwasiliana na mwenzake, kati ya Makamba na Mo.

Mo Dewji alitekwa Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Colosseum alikokwenda kwa ajili ya kufanya mazoezi na kupatikana Oktoba 20 saa nane usiku, baada ya waliomteka kumtelekeza katika viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam.