- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI LAMUACHIA DR LOUIS SHIKA '900 ITAPENDEZA ZAIDI'
Dar es salaam: Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limemuachia huru mnunuzi feki wa nyumba za Lugumu Dr. Louis Shika kwa dhamana ya kujidhamini mwenyewe baada ya kukosa mtu wa kumdhamini mnunuzi huyo.
akizungumza kwa njia ya simu na Muakilishi Media kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa "uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili Dr Louis Shika unaendelea lakini mpaka dakika hii hakupatikana mtu wa kumuwekea dhamana mtuhumiwa, sasa hatujui anaishi mwenyewe au laa" aliongea Mambosasa
Jeshi la polisi lilimtia nguvuni Dr. Louis shika kwa kosa la kuvuruga mnada kwa makusudi wa kutaka kununua nyumba za mfanyabishara mashuhuri nchini Bw. Said Lugumi mna tarehe 9.11.2017.Shika amekuwa mtu maarufu katika mitandao ya kijamii baada ya kufanyika kwa tukio la kutaka kununua nyumba hizo kwa mbwembwe za aina yake za kupandisha bei za nyumba hizo, msemo maarufu ni kama "mia 900 itapendeza zaidi" huku akiwa amevalia viatu vya wazi vinavyoonekana vimechakaa.