- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI LAENDELEA KUMSHIKILIA MBUNGE ZITTO KABWE
Dar es salaam: Mbunge wa Kigoma Mjini, na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe leo Novemba 1, 2018 ameondolewa kituo cha Oysterbay alikokuwa amehifadhiwa na kupelekwa Mahabusu ya kituo cha polisi Mburahati kilichopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Uamuzi huo umekuja baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake kuanzia saa 2:20 asubuhi hadi saa 5:45 na kumrudisha tena kituo cha Oysterbay.
Wakili wa Zitto, Jebra Kambole amesema kwamba wapo kwenye mchakato wa kuwasilisha maombi ya dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili mteja wao apate dhamana.
“Tupo kwenye hatua za mwisho za kuwasilisha maombi ya dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili mgeja wetu aweze kupewa dhamana,” ameeleza Kambole.
Zitto alikamatwa jana saa 5 asubuhi kwa madai ya polisi kuwa anakwenda kuhojiwa Juu ya mauaji ya Polisi na Raia 100 yaliyotokea kwenye Kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma.
Jana Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma lilimtaka mbunge huyo kudhibitisha mbele ya Jeshi hilo kwa kuwasilisha vielelezo vya madai yake kuwa yametokea mauaji eneo la Nguruka wilayani Uvinza mkoani humo na watu 100 walifariki Dunia.
Kama utakumbuka juzi siku ya Jumapili Oktoba 28,2018, Mbunge huyo alizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na kudai kuwa takribani siku 10 zilizopita yalitokea mauaji hayo na taarifa alizonazo ni kuwa watu zaidi ya 100, wakiwamo polisi walikufa.
Lakini kwaupande wa Jeshi hilo Jumanne, Oktoba 30, 2018, Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha tuhuma alizotoa Zitto na kusema hazina ukweli wowote.
Alisema hakuna watu 100 waliouawa na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.
“Hakuna watu mia moja waliouawa. Tunamtaka Zitto aonyeshe vielelezo vya hayo anayosema au aje atuonyeshe makaburi ya watu hao anaosema wameuawa Kigoma, ”amesema Ottieno