Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:54 am

NEWS: JESHI LA POLISI DOM LANASA WATUHUMIWA ZAIDI YA 120.

DOM: Jeshi La Polisi Mkoa Wa Dodoma Limekamata Watuhumiwa Zaidi Ya 120 Wanaojihusisha na Matukio Mbalimbali Ya Kiuhalifu Yakiwemo Kugushi Risiti Za Efd Na Tiketi,Wizi Wa Pikipiki na Wizi Wa Mifugo.

Kukamatwa Kwa Wahalifu Hao Kunafuatia Oparesheni Vunja Vijiwe Inayoendelea Mkoani Dodoma Na Katika Wilaya Zake.

Akitoa Taarifa Ya Jeshi Hilo jana Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Dodoma Gilles Muroto Amesema Kukamatwa Kwa Watu Hao Kumetokana Na Kazi Kubwa Inayofanywa Na Jeshi Hilo Kwa Kukamata Na Kuzuia Uhalifu Mkoani Hapa.

Aidha Kamanda Muroto Amesema Jeshi Hilo Pia Limefanikiwa Kumkamata Barack Jackob Masanja Aliyetoroka Na Sare Za Jeshi Kambi Za Jkt Rwamkoma Mara, Kwa Kujifanya Askari Wa Jkt Na Kuwatapeli Watu Akidai Kuwa Anawatafutia Ajira Jeshini Na Kuwatoza Fedha, Ambapo Kamanda Ametoa Rai Kwa Wananchi Kuwa Makini Na Matapeli Wanaojifanya Wana Uwezo Wa Kuawatafutia Ajira Jeshini.

Kamanda Muroto Amesema Kutokana Na Mkoa Wa Dodoma Kuwa Na Fursa Nyingi Wapo Watu Wanaokuja Kwa Ajili Ya Kutenda Uhalifu Ambapo Amesema Jeshi La Polisi Litaendelea Kupambana Nao Na Kuhakikisha Uhalifu Unakomeshwa Mkoani Hapa Pamoja Na Ndani Ya Wilaya Zake.

Akizungumzia Oparesheni Ya Vunja Vijiwe Kamanda Muroto Amesema Wtaendelea Kuvunja Vijiwe Hivyo Sambamba Na Kuwasambaratisha Wanawake Wanaojihusisha Na Biashara Ya Kuuza Miili Yao Ambapo Mpaka Sasa 17 Tayari Wamepelekwa Mahakamani