- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI DOM LAKAMATA WATUHUMIWA 46.
DODOMA: Jeshi la polisi mkoaniDodoma linawashikilia watuhumiwa 46 kwa kukutwa na makosa mbalimbali ikiwemo la kumiliki silaha kinyume na sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa kamanda wa polisi mkoa wa dodoma Gilles Muroto amesema msako uliofanyika wilaya ya Dodoma mjini alifanikiwa kukamata shehena kubwa ya umeme aina ya shaba zilizochunwa ganda la nje na nyingine kuchomwa moto na kupoteza uhalisia.
‘’Jumla ya viroba vikubwa na vidogo 26 vimekamatwa,’’amesema.
Amesema miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwakatika wilaya ya Kongwa alikamatwaTegemea Msauge miaka 34 mkazi wa kijiji cha Iduo tarafa ya Mlali akimiliki silaha moja aina ya Pistol iliyotengenezwa kienyeji na bila kibali.
Amesema wilaya ya Nchemba alikamatwa Hassan Ally miaka 22 mkazi wa kijiji Soya akiwa na noti bandia 50 za Sh 10000 sawa Sh 500000 hanzo cha kumatwa kwake alikutwa akizitumia kupatia huduma mbalimbali halali kwa kutumia fedha bandia kwa muda mrefu.
Akifafanua zaidi amesema miongoni mwa vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na pikipiki za wizi mbili namba Mc. 912 Atp aina ya boxer, Mc.806 Bmk boxer zote rangi nyeusi ,mitambo mine ya gongo (pombe haramu ya moshi) ns vipips vitatu na pombe haramu ya moshi lita 34 na bhangi misokoto 77 , bhangi kete 230 na bhag iliyosindikwa kilogram mbili.
Mbali na hayo kamanda huyo amesema kuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mkoa huo pamoja na kuimarisha doria lengo likiwa ni kudhibiti matukio ya uhalifu hasa kipindi hiki ambapo vikao vya Bunge vinafanyika mjini Dodoma.
Hata amesema jeshi hilo limejipanga kikamilifu kuhakikisha ulinzi unakuwepo wa kutosha hasa kipindhi hiki ambapo vikao vya bunge vinaendelea hapa mjini Dodoma.