- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA POLISI DODOMA LANASA WATUHUMIWA 15.
DODOMA: Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limekamata watuhumiwa 15 kwa makosa mbalimbali katika msako wake wa kuhakikisha mkoa unakuwa shwari kuelekea maadhimisho ya siku ya uhuru 9 Desember ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani humo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto akitoa taarifa hiyo amesemajeshi hilo limekuwa likufanya msako kupambana nakuongezeka kwa uhalifu katika kipindi hiki ambacho serikali inahamia makao makuu na shuguli mbalimbali za kitaifa zinazofanyika Dodoma.
Msako huo utahusisha maeneo yote zikiwemo nyumba za kulala wageni, stendi ili kuhakikisha hakuna wahalifu wanaoweza kutumia mwanya wa sherehe hizo kuingia Dodoma na kufanya matukio ya uhalifu.
Katika watuhumiwa hao 15 waliokamatwa kamanda Muroto amesema watuhumiwa watatu wamekutwa na jino la tembo lenye kilo 15 na mtuhumiwa mmoja akishikiliwa kwa kosa la udanganyifu na kujipatia kiasi cha zaidi ya shilingi million 20 huku wengine wakiwa na makosa ya usalama borabarani.
Katika kipindi cha jauari hadi October jumla ya watuhumiwa 521 wamehukumiwaadhabu mbalimbali mahakamani kutokana na kukutwa na hatia katika makosa mbalimbali waliyokuwa wakituhumiwa.