- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JESHI LA CHINA LAJIANDAA KUVISHAMBULIA VISIWA VYA MAREKANI
Jeshi la China linafanya mazoezi ya kujiandaa kushambulia vituo vya Marekani na vya washirika wake huko Pacific, kwa mujibu ya makao makuu ya ulinzi ya Marekani.
Katika Ripoti ya kila mwaka ya Congress inasema kuwa China inaongeza uwezo wake wa kupeleka ndege za kivita kwenye visiwa vyake vya baharini
Ripoti hiyo inazungumzia kuongezeka uwezo wa kijeshi wa China ikiwemo bajeti kubwa ya dola bilioni 190, thuluthi ya ile ya Marekani.
lakini China yenyewe bado hijazungumzia ripoti hiyo.
Onyo kuhusu mashambulizi ya angani ni moja ya malengo ya kijeshi na kiuchumi ya China.
"Kwa miaka mitatua iliyopita PLA [People's Liberation Army] limepanua maeneo yake ya kufanyia mazoezi bahrini, na kupata ujuzi wa maeneo muhimu ya baharini na kuna uwezekazo kuwa linafanya mazoezi kushambulia vituo vya Marekani na vya washirika," ripoti hiyo ilisema.
Inaendelea kusema kuwa haijulikani ni kipi China inataka kudhibitisha kwa kufanya mazoezi kama hayo.
"PLA huenda linataka kuonyesha kuwa lina uwezo wa kushambulia Marekani na vikosi washirika kwenye kambi za jeshi magharibi mwa bahari ya Pacific ikiwemo Guam," ripoti hiyo iliongeza.
Ripoti hiyo inasema kuwa China inapanga vikosi vyake "kupigana na kushinda".
"Lengo na mabadiliko haya ni kubuni kikosi hatari kinachozunguka ambacho kitakuwa nguzu ya oparesheni zake," kwa mujibu wa ripiti hiyo.
Bajeti ya jeshi la China inatarajiwa kuingezeka hadi dola bilioni 240 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Maeneo yenye misuko suko ni yapi?
Marekani ina wasi wasi kuhusu kuendelea kukua kwa China huko Pacific ambapo Marekani bado ina ushawishi mkubwa.
Kati maeneo ambapo mvutano upo ni kusini mwa bahari ya China ambalo ni eneo linalodaiwa na China na nchi zingine.