Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:42 am

NEWS: JELA MIAKA 60 KWA KUMBAKA MWANAFUNZI KIDATO 1

Kilimanjaro: Mahakama ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro leo Octoba 22 imemhukumu kifungo cha miaka 60 jela Abrahamu Kaaya (23) ambae ni mkazi wa kijiji cha Karansi wilayani Siha kwa makosa mawili ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Karansi.

Huku hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Jasmine Abdul baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi watano.

Kwamujibu wa Mwendesha mashtaka wa Serikali, Simoni Feo amesema mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 11, 2017 katika kijiji hicho.

Mwendesha mashtaka huyo aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.