- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JELA MIAKA 24 KWA KOSA LA KUWAAMBUKIZA WATU 30 UKIMWI
Italia: Mwanaume mmoja nchini Italia amekwenda jela miaka 24 kwa kosa la kuwaambukiza kwa makusudi wanawake wapatao 30 virusi vya Ukimwi.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 33 kwa jina la Valentino Talluto anadaiwa kufanya mapenzi bila kutumia kinga na wanawake zaidi ya 53 baada ya kugundulika kuwa ana virusi vya Ukimwi tangu mwaka 2006, mwanamke mdogo zaidi miongoni mwa hao alikuwa na miaka 14 wakati wa kuanza uhusiano wao.
Talluto ambaye kitaaluma ni Mhasibu ambaye alikuwa anatumia "Hearty Style", katika mitandao ya kijamii na tovuti za kuchumbiana kuwawinda waathiriwa wake.
Sasa siuku ya Ijumaa, jaji alimhukumu mwanamume huyo wa miaka 33 kifungo cha miaka 24 jela.
Mawakili wa Talluto walikuwa wametetea mteja wao wakisema vitendo vyake vilikuwa "visivyo vya busara, lakini havikuwa makusudi."
Hata hivyo, aliwaambia wale waliomwambia avalie mpira wa kondomu aliwaambia kwamba alikuwa na mzio, au kwamba muda mfupi awali alikuwa amepimwa na kupatikana hana Ukimwi, shirika la habari la AFP linasema.
Baadhi ya wanawake walipomkaripia baada ya kugundua kwamba walikuwa wameambukizwa, alikanusha madai kwamba alikuwa na virusi hivyo ambavyo husababisha Ukimwi.
Kutokana na vitendo vyake, watu wengine wanne waliambukizwa virusi hivyo kando na wanawake ambao aliwaambukiza moja kwa moja: wanaume watatu na mtoto mmoja.
Mwendesha mashtaka Elena Neri aliambia mahakama mwezi uliopita kwamba: "Vitendo vyake vilikusudiwa kupanda mauti."
Mamake Talluto alikuwa anatumia madawa ya kulevya na aliuambukizwa pia virusi vya Ukimwi.