- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAMII YATAKIWA KUWAENZI WATOTO
DODOMA: Ili watoto kuwa na maadili mazuri jamii inatakiwa kushirikiana na walimu , wazazi na walezi ili kupata viongoziwaaminifu wenye nidhamu na maadili ya kiroho.
Hayo yalisemwa na mstahiki meya wa manispaa ya Dodoma Profesa David Mwamfupe wakati wa mahafali ya 13 ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya wasichana huruma yaliyofanyika mjini hapa.
‘’Jukumu la malezi kwa watoto siyo la walimu peke yao bali ni ushirikiano kati yao’’, alisema.
Mbali na hayo Mwamfupe alisema serikali inaendelea kutambua na kuthamini mchango wa taasisi na mashirika ya kidini kwa kazi zuri zinazofanywa kwa kutoa michango yao katika kuunga mkono sekta ya elimu.
‘’Serikali bado inathamini michango mbalimbali ya taasisi ya mashirika ya kidini i inayotolewa ikiwemo ya kielimu, kiafya na maji’’, alisema.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Chrispiana Ikaku aliwataka wanafunzi kuhakikisha wanawekeza kwenye elimu ili kuweza kufikia malengo yao yatakayo wasaidia kupambana nachangamoto ya soko la ajira.
‘’Elimu mliyofikia ni mlango mwingine wa kujiendeleza zaidi, hivyo ili mweze kukabiliana na changamoto hiyo ni muhimu kujiepusha na vishawishi vinavyoweza mkajikuta mnaishi vijiweni’’, alisema.