Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:43 pm

NEWS: JAMII YATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KUDHIBITI USUGU WA VIMELEA VYA MAGONJWA.

DODOMA: Jamii nchini imetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti usugu wa vimelea vya magonjwa kwa lengo la kulinda Afya ya Binadamu,Mifugo na Mazingira na kukabiliana na mlipuko wa magonjwa yatokanayo na matumizi ya lishe isiyo bora au vyakula vyenye madawa na kemikali.

Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi barani Afrika zinazoendelea ambapo kumekuwa na vyakula mbalimbali vinavyoingia nchini ambapo changamoto kubwa inatajwa kuwa ni wingi wa kemikali na madawa yanayochanganywa katika vyakula

Akizungumza mara baada ya warsha ya udhibiti usugu wa vimelea Mtafiti kutoka Chuo cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof Robnson Ndegela amesema kuwa matumizi ya vyakula vyenye madawa ni moja ya changamoto ambapo wananchi wametakiwa kuzalisha kwa njia mbadala zisizotumia madawa

Gaudensia Semwanza ni Meneja wa mawasiliano kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA amesema kuwa mamlaka hiyo inapambana kwa kudhibitii vimelea vinavyoathiri chakula kwa kutumia maabara ya chakula na dawa na kudhibiti matumizi ya vyakula hivyo

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi mkoani Dodoma wamesema kuwa ipo haja ya serikali kuendelea kutoa Elimu kwa jamii ili kudhibiti matumizi ya vyakula visivyo na ubora pamoja na kutafuta njia nyingine mbadala za uzalishaji


Usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa hutokea pale ambapo vimelea hivyo vinabadilika na kuwa sugu kwa dawa zinazotumika kwa matibabu ambapo mwito unatolewa kwa wadau kuhakikisha wanaepuka matumizi ya vyakula ambavyo havina ubora