Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 12:44 pm

NEWS: JAMII YATAKIWA KUMUENZI HAYATI MWALIMU NYERERE KWA VITENDO.

DODOMA: Watanzania mkoani Dodoma wameungana katika kuadhimisha kumbukizi ya miaka 18 ya kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya kwanza Hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere huku jamii ikitakiwa kuenzi kwa vitendo fikra na harakati za kiongozi huyo katika kudhibiti vitendo vya ubadhilifu,rushwa na uzalendo katika kuleta maendeleo nchini.

Maadhimisho hayo ambayo yameenda sambamba na kufunga kilele cha mbio za mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa visiwani Zanzibar ambapo mkoani Dodoma jumuiya ya wanataaluma wa chuo hicho wameungana katika maadhimisho hayo yakienda sambamba na maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa chuo hicho

Akizungumza katika maadhimisho hayo Makamu Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM Prof Idriss Kikula amesema kuwa enzi za uhai wa mwalimu Nyerere alikuwa mstari wa mbele katika kudhibiti ubadhilifu na ufisadi hivyo watanzania wanapaswa kuenzi kwa vitendo .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho ya miaka 10 ya chuo hicho Prof Julius Nyahongo amesema kuwa chuo kikuu cha Dodoma kinatambua umuhimu wa baba wa taifa katika kupigania maslahi ya taifa na kusimamia maadili na uzalendo kwa viongozi na watanzania


Shukuru Mlawafu ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanataaluma ambapo amesema kuwa kupitia maadhimisho ya miaka 18 tangu kifo cha baba wa taifa watanzania wanapaswa kutambua kuwa baba wa taifa alikuwa na mchango mkubwa katika kusimamia maadili kwa taifa na kupambana na maadui watatu Ujinga,Umaskini na maradhi

Maadhimisho hayo yaliyoenda sambamba na zoezi la uchangiaji wa damu pamoja na kutolewa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi hiyo yote ikiwa ni katika kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere