- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAMII YATAKIWA KULINDA AMANI.
JIJINI DOM: MKURUGENZI wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali, inayojihusisha na Vijana (DOYODO)Rajabu Selemani amesema kuwa wapo watu wengi wanaonekana machoni wana amani kumbe moyoni hawana amani.
Mbali na hilo mkurugenzi huyo amesema masuala ya amani yasichukuliwe kama sehemu ya kuzuia vurugu au machafuko ambayo yanaonekana machoni lakini amani pia ionekane ni namna gani Vijana au jamii ilivyo na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.
Ametoa kauli hiyo leoJijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupu baada ya Mustafa Hasani kutoa kituo cha habari cha umoja wa mataifa akimwakilisha Stella Vuzo, kusoma taarifa juu ya maadhimisho ya siku ya Amani duniani.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa licha kuwepo kwa uhamasishaji wa kina, Amani ya nchi na duniani kwa ujumla ni vyema kuangalia kwa mapana zaidi badala ya kufikiria zaidi katika vurugu.
"Mimi ninapoangalia juu ya utunzaji wa Amani naliona jambo hili kwa namna tofauti zaidi jambo la kwanza ni lazima tuangalie watu wana amani kiasi gani moyoni.
Kwa upande wake Mustafa Hasani kutoka kituo cha habari cha Umoja wa mataifa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya siku ya amani Duniani amesema katika kuhakikisha amani inalindwa vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza amani ya nchi.
Amesema ili kuhakikisha vijana wanatunza amani ya nchi wameandaa kongamano lenye ujumbe usemao "haki ya kuwa amani miaka 70 ya Azimio la ulimwengu la Haki za Binadamu".mwaka 2018".
Naye Ofisa Maendeleo ya vijana Mkoa wa Dodoma Tumsifu Mwasamale akizungumza na vijana amesema pamoja na juhudi za kuhamasisha amani lakini jamii inatakiwa kutambua kuwa ni muhimu kuwaombea viongozi wa mataifa makubwa Marekani na Korea kwa madai kuwa ndiyo wameshikilia amani ya Dunia.
Amesema kuwa hatua ya Rais wa Marekani na Rais wa Korea kukutana na kujadiliana masuala ya amani na kukubaliana ni ishara tosha kuwa amani inasimama kwenye mstari hivyo wanatakiwa kuombewa.
Mbali na hilo amewataka vijana kilinda amani ya nchi na wasikubali kutumiwa kisiasa huku akiwataka kulitumia Jiji la Dodoma kama kisiwa cha amani.