- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAMII YATAKIWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI ZIDI YA WATOTO WA KIKE.
DODOMA: Mikoa ya Dodoma na Singida imeungana kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani huku jamii ikitakiwa kufichua vitendo vya ukatili kwa mtoto wa kike na changamoto zinazosababisha mtoto wa kike asifikie malengo yake ikiwemo mimba za utotoni,ndoa za utotoni,ukeketeaji na ubakaji pamoja na kukosekana kwa miundombinu ya kujistiri wakati wa hedhi.
Maadhimisho hayo yanayofanyika kitaifa mkoani Tarime yana lengo la kumwondoa mtoto wa kike katika hatari ya kupata mimba za utotoni ambapo Kaulimbiu ya siku ya mtoto wa kike mwaka huu inasema tokomeza mimba za utotni,tufikie uchumi wa viwanda
Akizungumza katika mdahalo uliohusisha wadau mbalimbali pamoja na wanafunzi wa shule za msingi kutoka mikoa ya Dodoma na Singida Afisa Elimu vifaa na takwimu mkoa wa Singida Zenaida Msita amesema watoto wa kike wamekuwa wakikosa haki zao za msingi hivyo kushindwa kutimiza ndoto zao za kimaisha.
Baadhi ya wanafunzi wa kike walioshiriki katika mdahalo huo wamesema ipo haja ya serikali kutatua changamoto zinazowafanya watoto wa kike kukosa haki zao za msingi ikiwemo kujengwa kwa chumba cha faraga kwa ajili ya mtoto wa kike kujistiri awapo shuleni
Baadhi ya wadau wa elimu akiwemo Mwalimu Leyla Ali amesema kuwa ili mtoto wa kike afikie ndoto zake jamii inapaswa kutambua umuhimu wa mtoto wa kike huku mmoja wa wazazi akisema kuwa wazazi wanatakiwa kuwa karibu na watoto na kuwapa elimu
Kila mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha mtoto wa kike anafikia ndoto zake za kimaisha.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo mjengee uwenzo mtoto Wa kike kabla na baada ya majanga shiriki kutokomeza vikwanzo vinavyomzuia mtoto Wa kike kufikia malengo yake ni pamoja na mazingira duni ya kujifunzia , ukosefu Wa huduma za mtoto Wa kike aliyepevuka awapo shuleni, ubakaji mimba za utotoni na kuwaonzesha mapema