Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:41 am

NEWS: JAMII YATAKIWA KUACHA UJENZI KATIKA MAENEO HATARISHI.

DODOMA: Watanzania wameungana na wenzao duniani katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupunguza maafa huku serikali ikiahidi kuendelea na operesheni ya kuwaondoa wananchi waliojenga makazi katika maeneo hatarishi kwa kutunga na kusimamia utekelezaji wa sheria ya mipango miji ya mwaka 2017.

Lengo la maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma ni kukuza utamaduni wa kupunguza madhara ya maafa kimataifa,ikiwa ni pamoja na kuzuia,kupunguza madhara,kujitayarisha,kukabili na kurejesha hali ya kuwa bora zaidi ili kupunguza madhara na hasara katika maisha.

Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho hayo kitaifa mkoani Dodoma Mkurugenzi msaidizi wa uratibu wa shughuli za maafa ofisi ya waziri mkuu Bashiru Taratibu amesema ili kupunguza ujenzi holela serikali imeendelea kuandaa mipango itakayoongoza uendelezaji na ukuaji wa mji


Baadhi ya wadau walioshiriki maadhimisho hayo wamesema madhara ya maafa ni makubwa pale yanapotokea hivyo jamii inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuchukua tahadhari ya maafa


Wakizungumza kwa nyakati tofautibaadhi ya wakazi mkoani Dodoma wamesema kuwa ipo haja kwa serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara yatokanayo na maafa


Oktoba 13 ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupunguza maafa ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Makazi salama,punguza makazi katika maeneo hatarishi,punguza kuhama kutokana na maafa
Mwisho