Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:23 pm

NEWS: JAMHURI YATOA USHAHIDI KIFO CHA MWANAFUNZI KAGERA

BUKOBA: Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba leo Septema 17, 2018 imeanza kusikiliza ushahidi wa upande wa jamhuri katika kesi ya mauaji ya mwanafuzi Sperius Eladius, aliyeuwawa kwa Kipigo kutoka kwa walimu wake wawili ambao ni Respickius Patrick na mwalimu Erieth Jeradi wote wakiwa walimu wa shule ya msingi kibeta.

Mwanafunzi huyo alifariki Agosti 27 na mwili wake kupelekwa katika hospitali ya Kagera

Awali, familia ya mtoto huyo ilisusia mwili wa mwanafunzi huyo baada ya uchunguzi uliotolewa na mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa Mkoa wa Kagera, Dk John Mwombeki kueleza kuwa mwili wake ulikutwa na alama zinazoonyesha alipigwa siku kadhaa kabla ya kukutwa na umauti.