Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 6:38 pm

NEWS: JAFO MGENI RASMI MAHAFALI YA CHUO CHA UALIMU CAPITAL DODOMA.

DODOMA: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI, Selemani Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasm katika mahafali ya 10 ya chuo cha ualimu caha Capital kilichopo Miyuji mjini hapa.

Licha ya kuwa mgeni rasm pia Jafo atakuwa na jukumu la kuwatunuku wanachuo wa chuo hicho 62 wanaohitimu ngazi ya Stashahada ya ualimu wa shule ya msingi.

Kwa mujibu wa mikuu wa Chuo hicho Khani Charokiwa amesema kuwa wameona ni vyema kumwalika Waziri huyo kwa lengo la kusikoliza chamgamoto mbalimbali ambazo vyuo binafsi wanakumbana nazo.

Hata hivyo amesema kuwa licha ya kuwa vyuo vingi vya binafsi kuwa na changamoto mbalimbali lakini bado wanawajibu mkubwa wa kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa wanavyuo ili kuweza kuboresha elimu ya motto wa kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Charokiwa amesema kuwa kati ya changamoto ambayo chuo chake kinakumbana nazo ni pamoja na idadi ya wanachuo kupungua kila mwaka kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya sifa za kujiunga katika vyuo.

Aidha amesema kuwa changamoto nyingine ni kufutwa kwa kozi ya ODPE, vyuo vya ualimu kuzuiwa kutoa mafunzo ya kozi nyingine mbali na ualimu, kutoajiliwa na serikali wahitimu wa ualimu kuanzia mwaka 2015 licha ya kuwa na uhaba wa walimu.

Amesema kitendo hicho kinawakatisha tama wale wenye ufaulu mzuri kusoma ualimu,ulipaji wa ada na michango ya chuo kwa wanachuo.

Kutokana na hali hiyo serikali inaombwa kutoa ajira kwa wahitimu wa ualimu ili wanafunzi waliofaulu vizuri wavutiwe kujiunga na vyuo vya ualimu.

Pia ni vyema serikali ikaona ni busara bodi ya mikopo kuwakopesha wanachuo wa ngazi ya stashahada ili kuwawezesha wasome vizuri.