Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 3:40 am

NEWS: JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUSIMAMIA VYEMA MATUMIZI.

GEITA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka viongozi wa Halmashauri nchini kusimamia matumizi ya mapato yanayokusanywa katika Halmashauri zao.

Jafo ametoa kauli hiyo alipokuwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Geita na Chato katika mkoani wa Geita.

Amesema Halmashauri mbalimbali zinatakiwa kusimamia vyema matumizi ya mapato hayo na kwa kiasi kikubwa yaelekezwe katika miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri hizo kwa maslahi mapana ya wananchi.

Waziri Jafo amepongeza viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato.

Katika ziara hiyo, Waziri huyo amefanikiwa kukagua ujenzi wa soko la kisasa linalojengwa kwa fedha za ndani za Halmashauri ya mji wa Geita, barabara za lami za mji wa Geita zinazojengwa kwa mradi wa ULGSP, zahanati ya Buselesele, Kituo cha Afya Bwanga kilichopo wilayani Chato, pamoja na kutembelea shule ya sekondari Magufuli.

Akiwa Buselesele, Waziri Jafo amewahakikishia wananchi wa kata ya Buselesele kwamba serikali itajitahidi ili ijenge kituo cha afya cha kisasa katika kata hiyo ya Buselesele kutokana na idadi kubwa ya wananchi katika eneo hilo.