- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO AWATIA MATUMBO JOTO WATAALAM WA KILIMO NCHINI
TABORA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameanza kuwapima wataalam wa kilimo kivitendo hapa nchini baada ya maelekezo yake aliyo yatoa miezi miwili iliyopita kwa wataalam wote wa kilimo hapa nchini kuwafikia wakulima kwa kuwapa elimu ya kilimo badala ya kukaa ofisini.
Lengo la agizo hilo ni kuongeza uzalishaji kwa kufuata kanuni za kilimo bora.
Akiwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Jafo amepata nafasi kutembelea mashamba ya wakulima na kubaini hawajapata ushauri wowote wa kitaalam.
“Inawezekana wataalam wengi wa kilimo wamechukulia poa agizo leo nimeanza ukaguzi mashamba nimefika hapa nimekuta mashamba yamepandwa hovyo hovyo bila kufuata kanuni za kilimo bora,”amesema
Kutokana na hali hiyo, Waziri Jafo aliwajia juu maafisa kilimo na kuwaonya kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Waziri Jafo ametoa onyo kwa afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya Nzega na kumtaka ajirekebishe kabla hajachukuliwa hatua kali za kiutumishi.