Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:32 am

NEWS: JAFO AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA HIYO KUJIPIMA KATIKA UTENDAJI KAZI.

DODOMA: Waziri wa Nchi ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka watumishi wote wa Wizara hiyo kujipima na kujitafakari katika utendaji wao wa kazi na wale wanaodhani hawawezi kufanya kazi kwa kasi ya sasa bora wakae pembeni.

Jafo ametoa kauli hiyo leo mjini Dododma wakati akijitambulisha kwa watumishi wa Wizara ya TAMISEMI baada ya kuapishwa kuwa Waziri kamili wa Wizara hiyo ambapo amesem hatovumilia watumishi ambao wanafanya kazi kwa mazoea na wasiojali muda

Pia Waziri Jafo amesikitishwa kuona shule za serikali za vipaji maalum kutokushika nafasi za juu katika mitiani ya kitaifa badala yake shule za binafsi ndizo zinafanya vizuri jambo ambalo halikubaliki.


Mbali na hayo Jafo amewakemea watumishi ambao badala ya kufanya kazi kwa ufasaha wamekuwa mabingwa wa kupika majungu kwa lengo la kuwagombanisha watumishi.


Waziri Jafo leo amezungumza na watumishi wa Wizara yake kwa mara ya kwanza toka ateuliwe kuwa waziri kamili wa wizara hiyo wiki iliyopita.