- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO AWATAKA WATENDAJI WA MANISPAA ZA DAR ES SALAAM KUONGEZA KASI YA UTENDAJI
DAR: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka watendaji wote wa Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam kuongeza kasi ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.
Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo inayo tekelezwa na serikali katika Manispaa hiyo.
Katika ziara yake leo ametembelea Manispaa ya Kigamboni na kukagua ujenzi wa Ofisi za Manispaa hiyo pamoja na ujenzi wa Kituo cha afya Kimbiji.
Katika miradi hiyo, Waziri Jafo hakufurahishwa na kasi ya ujenzi wa Miradi hiyo ya maendeleo huku akiagiza ujenzi wa Ofisi za Manispaa ukamilike kabla mwezi Januari mwaka 2019 ili waondokane na tatizo la kupanga kwenye nyumba ya mtu binafsi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda amemuahidi Waziri Jafo kwamba wao kama mkoa wamejipanga kutekeleza maagizo yote na kuwataka watumishi wote wa mkoa huo kubadili utendaji kazi wao ili kutekeleza kwa wakati miradi.