Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:26 pm

NEWS: JAFO AWATAKA VIONGOZI KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA KWAVITENDO.

DODOMA: Waziri Wa Tamisemi Selemani Jafo amewataka wakuu Wa wilaya,mikoa na wakurungezi kufanyakazi kwa weledi na kwa vitendo ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika kazi.

Jafo ameyasema hayo Wakati akifungua mkutano Wa thamini ya dhana ya kung'atukaji Wa madaraka na uboreshaji wa huduma kwa watumishi wa umma,wakuu wa wilaya,wakurugenzi na wa wakuu wa Mikoa.

Aidha amewataka watendaji hao kujadili kwa kina mijadala hiyo ili kuleta mabadiliko katika sekta ya umma na uwajibikaji maboresho.

"Eneo la muhimu la kufanyia maboresho ni uchumi ili kuboresha uchumi Wa nchi lazima mapindunzi yafanyike katika sekta ya umma,"amesema.

Pia aliwataka watumishi hao kutofanya kazi kwa mazoea ili kuleta maendeleo katika jamiii na kufikia uchumi Wa kati na wa viwanda.

" Leo hii kuna watu wanaenda likizo lakini ndani ya ofisi yake hakuna mtu anayejua ameenda likizo,"amesema.

Miongoni mwa agenda hizo in pamoja na maboresho katika utumishi Wa umma, Matumizi ya tehama ndani ya kazi.

Awali akizungumza naibu katibu mkuu Wa Tamisemi Tixon Nzunda amesema baada ya kufanya tathimini ya ung'atukaji Wa madaraka utafiti unalenga kuboresha utekelezaji wa sera.

Hata hivyo ameongeza kuwa baada ya utafiti huo utaboresha taifa na kutoa muelekeo Mpya Wa mkakati.