Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:52 am

NEWS: JAFO AWAONYA WAFANYABIASHARA WA MBEGU

DODOMA: Katika kuelekea msimu wa kilimo Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo amewataka wafanyabiashara wa mbegu nchini kuacha kuwauzia wakulima mbegu feki na matokeo yake kuwauzia mbegu zenye ubora ili kulinda maslahi ya wakulima.

Jafo ameyasema hayo leo wakati wa kufunga warsha ya wadau wa mbegu Tanzania iliofanyika mjini Dodoma .

Amesema kitendo cha kuwauzia wakulima mbegu zisizo na ubora kunawasababishia hasara na matokeo yake kushindwa kujikwamuwa kiuchumi.

‘’Mbegu feki zimetapakaa kote nchini kamahakuna jukwaa la kusimamia hili Taifa linaweza kufikia pabaya;’’amesema.

Aidha amesema kuwa changamoto kubwa zinazowakabili wakulima hapa nchini ni uhaba wa fedha jambo ambalo limekuwa chanzo cha wakulima kuchanganya mbegu zaidi ya moja ambazo hazina ubora na kuwasababishia kupata mazao hafifu .

Jafo amesema kuwa wazalishaji wa mbegu hapa nchini wamekuwa wachache huku idadi ya watumiaji wa mbegu kuongezeka jambo ambalo kuchangia wakulima kushindwa kupata mbegu kwa wakati.

Ameongeza kuwa changamoto nyingine ni pamoja na mfumo finyu wa usambazaji , miundombinu duni, gharama kubwa ya unununuzi wa mbegu kwa wakulima na kukosekana kwa chombo ambacho kingeweza kuwaleta na kuhakikisha utendaji wao.

Mbali na hayo ametoa wito kwa wadau wa jukwaa hilokuhakikisha mifumo yote ya sekta ya mbegu inafanyika vizuri na kwa weledi ili kutatua changamoto ya mbegu feki nchini.

‘’Hali ya wakulima wetu uchumi wao ni mdogo sana fikiri ni hasara kiasi gani wanapata lakini bado wanaendelea kupambana,’’amesema.

Lengo la warsha hiyo ni kusimamia masuala yote yanahusu mbegu nchini yatakayowezesha (uhakika wa upatikanaji ,unafuu na ubora)ambapo Warsha hiyo iliandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi za Kiraia ,Ansaf pamoja na Toam kwa hisani ya Taasisi ya Resalux ya Ujerumani.