- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO ASEMA HATAMVUMILIA YEYOTE ATAKAYEHUSIKA NA RUSHWA TARURA.
MWANZA: Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amewaonya watumishi wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini(TARURA) mikoani na wilayani kutojihusisha na masuala ya Rushwa wakati wanatimiza majukumu yao kwa kuwa watakaojihusisha watachukuliwa hatua kali zikiwemo kutimuliwa kazini.
Jafo aliyasema hayo alipokuwa anafunga mafunzo hayo jijini mwanza kwa maafisa wa TARURA wa wilaya na mikoa kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ikihusishwa Mwanza, Mara, Shinyanga, simiyu, Geita, kagera, Kigoma, na Tabora.
Katika mafunzo hayo,washiriki wa mafunzo hayo wamejengewa uwezo katika swala la manunuzi, mikataba, maadili, Rushwa, Jinsia, Ukimwi, pamoja na afya na usalama mahala pa kazi.
Mafunzo kama haya yamesha kamilika katika kanda zingine za kaskazini, na kanda mashariki na Kati na yanatarajiwa kukamilishwa kwa mikoa iliyobaki ya kanda za juu kusini mwanzoni mwa mwezi Januari 2018.