- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO AISHUKIA MANISPAA YA ILALA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI
DAR: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amechukizwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Ilala.
Jafo ameonyeshwa kukerwa wakati alipokuwa katika ziara ya Kikazi Mkoani Dar es salaam katika Manispaa ya Ilala.
Katika Ziara hiyo, Waziri Jafo ametembelea Machinjio ya Vingunguti ambayo hivi kalibuni ilitengewa fedha shilingi bilioni 8 kwa ajili ya kujenga machinjio ya Kisiasa pia ametembelea Kituo cha afya cha Mnyamani ambacho kimepewa fedha shilingi milion 500 pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Kivule.
Jafo ameonyeshwa kutofurahishwa na kusuasua kwa miradi hiyo kwani ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti haujaanza hadi sasa licha ya kupokea fedha za awali zaidi ya shilingi bilion tatu zaidi ya miezi mitatu iliyopita.
Pia amebaini kasi ndogo ya ujenzi wa miundombinu katika Kituo cha afya Mnyamani licha ya kupokea fedha tangu mwanzoni mwa mwezi Juni 2018.
Kutokana na hali hiyo,Waziri Jafo amemtaka Mkurugenzi Mpya wa Manispaa hiyo Jumanne Shauri kubadilisha kasi ya utendaji katika Manispaa hiyo ili fedha za Serikali ziweze kuleta mabadiliko yanayokusudiwa katika Manispaa hiyo.
Aidha, Waziri Jafo amewashangaa viongozi na watendaji wa Manispaa hiyo kwa kutotoa fedha zozote kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Kuvule kitendo kilichosababisha ujenzi huo kusimama kwa zaidi ya miaka miwili wakati manispaa hiyo imekusanya zaidi ya shilingi bilion 44 katika mwaka wa fedha 2017/2018 kutoka vyanzo vyake vya ndani.
Jafo ameelezea kwamba Serikali kuu imetenga fedha shilingi bilioni 1.5 katika bajeti ya mwaka huu 2018/2019 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Kivule lakini ameitaka manispaa hiyo kuacha kubweteka kwa kutegemea fedha za Serikali kuu pekee wakati manispaa hiyo ina uwezo mkubwa wa mapato.