Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:46 am

NEWS: JAFO AAGIZA WEZI WA VIFAA VYA UJENZI KITUO CHA AFYA NDAGO WAKAMATWE

IRAMBA SINGIDA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida kupitia vyombo vya dola kuwasaka wezi wote waliiba vifaa vya ujenzi wa kituo cha afya Ndago wilayani huo na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Jafo ametoa agizo hilo leo baada ya kufanya ziara katika Kituo cha afya Ndago ambacho ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyopokea Sh.Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali lakini ujenzi wake haujakamilika hadi sasa kutokana na baadhi ya vifaa kuibwa na wananchi wasio waaminifu.

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ameonyesha kukerwa na uzembe wa usimamizi uliojitokeza katika ujenzi wa kituo hicho cha afya.

Hata hivyo, pamoja na kuagiza kusakwa kwa wezi wa vifaa, Waziri Jafo ameiagiza Ofisi ya mkoa wa Singida kufanya uchunguzi ndani ya wiki moja ili kubaini kama kuna watumishi waliohusika katika sakata hilo nao wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.

Waziri Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba kukamilisha ujenzi wa majengo hayo kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Agosti ili wananchi wa Ndago waweze kupata huduma bora ya afya kama ilivyokusudiwa na serikali.

Aidha katika ziara hiyo waziri Jafo ametembelea na kukagua pia ujenzi wa barabara mpya ya kilometa 10 inayotoka Kiengege kwenda kata ya Ndago ambapo amepongeza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA) kwa kazi nzuri waliyoifanya katika ujenzi wa barabara hiyo