Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 6:48 am

NEWS : ISRAEL YAWATIMUA WAHAJIRI 38,000 KUTOKA NCHI ZA AFRIKA

Israel yawatimua wahajiri 38,000 wa Kiafrika

Israel yawatimua wahajiri 38,000 wa Kiafrika

Utawala wa Kizayuni wa Israel umeanza kutekeleza mpango wa kuwarejesha nchini kwao kwa nguvu makumi ya maelfu ya Waafrika walioingia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ameliambia baraza lake la mawaziri kwamba utekelezwaji wa mpango huo ulianza jana Jumatano.

Amesema wahajiri haramu 38,000 wa Kiafrika wana hadi mwezi Machi mwaka huu kuondoka kwa khiari, vinginevyo watakamatwa.

Mpango huu ambao uliidhinishwa na baraza la mawaziri la Israel mwezi Novemba mwaka jana uliibua malalamiko kutoka taasisi nyingi za kimataifa likiwemo Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja UNHCR.

Wahajiri wa Kiafrika wanaozuiliwa katika jela za Israel

Wengi wa wahajiri hao ni kutoka Sudan na Eritrea na wamekuwa wakiingia katika ardhi hizo za Palestina kupitia mpaka wa jangwani na Misri.

Israel inadai kuwa imeafikiana na viongozi wa Rwanda na Uganda juu ya kuwakabidhi wahajiri hao kwa nchi hizo za mashariki mwa Afrika.