- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : ISRAEL YAKAMATA WANAHARAKATI NA BOTI ZAO HUKO UKANDA WA GAZA
Vikosi vya baharini vya utawala wa Kizayuni wa Israel jana vimeusimamisha msafara wa boti za wanaharakati wa Kipalestina waliokuwa na nia ya kuvunja mzingiro wa kidhalimu wa miaka 11 katika Ukanda wa Ghaza.
Salah Abd al-Ati, mmoja wa wanaharakati walioratibu msafara huo wa amani ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, wanajeshi wa Israel wamewakamata wanaharakati 17 katika uvamizi huo, mbali na kushikilia boti zao.
Amesema, "Msafara wetu ulizingatia kanuni zote za haki za binadamu zinazowapa kibali cha kusafiri. Ghaza inasalia kuwa gereza kubwa la wazi lililotelekezwa, na wala haipokei haki zake za msingi kutokana na mzingiro wa Israel."
Kabla ya kuvamia msafara huo wa amani, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zilitekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, baada ya wanamuqawama wa Palestina kuvurumisha maroketi 22 kuelekea Israel kufuatia hujuma ya makombora ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya vituo vya harakati za kupigania ukombozi Palestina.
Katika uvamizi huo wa Israel huko Ghaza hapo jana, Mpalestina mmoja aliuawa shahidi huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.
Tangu Januari mwaka 2006 na kufuatia ushindi wa harakati ya Hamas katika uchaguzi wa Bunge la Palestina, utawala wa Kizayuni wa Israel uliliwekea eneo la Ukanda wa Ghaza mzingiro wa angani, baharini na nchi kavu kwa lengo la kuisambaratisha harakati hiyo ya muqawama. Mzingiro huo unazuia kuingizwa katika eneo la Ghaza bidhaa za mahitaji ya msingi zikiwemo za fueli, dawa na vifaa vya ujenzi.