Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 6:31 am

NEWS : IRANI YASEMA SAUDIA INAUA RAIA WENGI YEMEN KWA VISINGIZIO VYA MAGENGE YA KIGAIDI

Iran: Saudia inaua raia wengi nchini Yemen, kuliko magenge ya kigaidiIran: Saudia inaua raia wengi nchini Yemen, kuliko magenge ya kigaidi

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema muungano vamizi wa kijeshi wa Saudi Arabia unaua idadi kubwa ya raia nchini Yemen kuliko magenge ya kigaidi.

Akihutubia Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Eshaq Al Habib amesema idadi ya raia hususan watoto wadogo wanaouawa katika mashambulizi ya Saudia ni kubwa mno ikilinganishwa na idadi ya watu waliouawa na magenge ya kigaidi ya Al-Qaeda, ISIS (Daesh) and Nusrah.

Amesema kitendo cha Riyadh kudai kuwa inaunga mkono jitihada za kimataifa za kupambana na ugaidi ni kejeli kwa ubinadamu, haki za binadamu, haki na amani.

Watoto wa Yemen, wahanga wakuu wa hujuma za anga za Saudia

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amebainisha kuwa, ni jambo lisiloingia akilini kwamba Riyadh inadai kupambana na ugaidi, wakati ambapo maafisa wake wa usalama wanaendeleza mauaji ya kimbari katika mji wa Awamiya, mashariki mwa Saudi Arabia.

Hii ni katika hali ambayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni alimuandikia barua Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akisema kuwa hali ya mambo nchini Yemen ni mbaya sana na inatia wasiwasi mkubwa