- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : IRAN YAIONYA SAUDI ARABIA KUHUSU UFITISHAJI AFRIKA MASHARIKI NA KATI
Iran yaonya kuhusu ufitinishaji wa Saudi Arabia Mashariki ya Kati
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena ametahadharisha kuhusiana na uropokaji, madai hayo kwa hayo na yasiyo na msingi na ufitinishaji wa viongozi wa Saudi Arabia katika eneo la Mashariki ya Kati.
Bahram Qassemi amekumbusha natija ya hatua za uharibifu za watawala wa Saudia katika eneo hili nyeti la Mashariki ya Kati na kubainisha kwamba, katika miaka ya hivi karibuni nchi za eneo hili hazijashuhudia kitu kingine kutoka kwa Saudia ghairi ya ukiukaji wa haki za binadamu, kuzusha fitina baina ya nchi za Kiislamu na Kiarabu, kukariri na kueneza madai ya uongo na yasiyo na msingi, kuzizingira kiuchumi nchi jirani, kuzitishia nchi nyingine na kuzitumbukiza katika vita vya ndani sambamba na kuzusha fitina za kikaumu, kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine, kuzishinikiza kisiasa na kadhalika.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema bayana kwamba, siasa kama hizi ni kengele ya hatari kwa nchi zote za Mashariki ya Kati na ulimwengu mzima kwa ujumla.
Ameongeza kuwa, walimwengu wanapaswa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na ufitinishaji wa Adel al-Jubeir, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudia.
Akizungumza hapo jana na waandishi wa habari mjini Riyadh akiwa pamoja na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa, Adel al-Jubeir Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia alidai kwamba eti Iran inaitumia Hizbullah ya Lebanon kwa ajili ya kupanua satwa na ushawishi wake katika eneo la Mashariki ya Kati