- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : IRAN NA MPANGO WA KUFUTA MATUMIZI YA DOLA KWENYE BIASHARA ZAKE
Iran kufuta sarafu ya dola ya Marekani katika biashara ya kimataifa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalenga kufuta kabisa matumizi ya dola ya Marekani katika biashara zake za kimataifa.
Hayo yamedokezwa na Msemaji wa Serikali ya Iran Bw. Mohammad Baqeri Noubakht Jumanne alipokuwa akizungumza na waandishi habari mjini Tehran. Amesema kwa miaka kadhaa sasa Iran imekuwa ikitekeleza mkakati maalumu wa kufuta dola katika mabadilishano yake ya biashara za kimataifa na kwamba hivi sasa inatumia zaidi sarafu ya Euro.
Aidha amesema Iran imefikia mapatano na baadhi ya nchi za eneo kama vile Jamhuri ya Azerbaijan na Russia ambapo katika mabadilishano ya kibiashara sarafu za kitaifa ndizo zitakazotumika.
Mwezi Septemba mwaka huu pia wakati wa safari ya Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki nchini Iran, nchi mbili zilifikia mapatano ya awali ya kutumia sarafu za kitaifa katika biashara baina yao badala ya kutegemea sarafu za kigeni.
Nchi kadhaa duniani zimeanza kuchukua hatua za kutupilia mbali sarafu ya Dola ya Marekani katika biasahra za kimataifa. China na Russia zimekuwa zikiongoza jitihada za kimataifa za kuondoa utegemezi wa sarafu ya Dola ya Marekani na kwa msingi huo kuanzisha mfumo mpya wa kifedha duniani.