Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:44 am

NEWS : IOM IMESEMA BAHARI YA MEDITERENIAN NDIO MPAKA UNAOUWA ZAIDI DUNIANI

IOM: Bahari ya Mediterania ndiyo mpaka unaoua idadi kubwa zaidi ya watu duniani

IOM: Bahari ya Mediterania ndiyo mpaka unaoua idadi kubwa zaidi ya watu duniani

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuwa, kuanzia mwaka 2000 hadi sasa zaidi ya watu elfu 33 waliokuwa katika jitihada za kuelekea Ulaya kupitia Bahari ya Mediterania wamepoteza maisha.

Jorge Galindo ambaye ni afisa wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji amesema katika mkutano unaofanyika mjini Geneva huko Uswisi kwamba, ripoti ya shirika hilo inaonesha kuwa, tangu mwaka 2000 hadi sasa watu wasiopungua 33 elfu na 761 wamepoteza maisha au wametoweka katika Bahari ya Mediterania na kwamba mpaka wa majini wa nchi za Ulaya kwenye maji ya bahari hiyo ndiyo wenye mauaji ya idadi kubwa zaidi ya watu duniani.

Prof. Philippe Fargues ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo cha Sera za Wahajiri cha Umoja wa Ulaya huko Florence nchini Italia ametahadharisha kuwa, kufungwa kwa njia fupi na zisizo na hatari za kuelekea Ulaya kumewalazimisha wahajiri kutumia njia zenye hatari kubwa na ndefu zinazozidisha hatari ya kifo.

Wahajiri katika maji ya Bahari ya Mediterania


Takwimu rasmi zinaonesha kuwa, mwaka huu wa 2017 pekee karibu watu elfu tatu wamefariki dunia au kutoweka katika maji ya Bahari ya Mediterania wakiwa katika mikakati ya kuelekea barani Ulaya.

Fargues ameongeza kuwa, takwimu rasmi haziakisi hali halisi ya maafa ya binadamu yanayotokea katika Bahari ya Mediterania.