Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:38 am

NEWS : IMEFAHAMIKA KUWA UKANDA WA GAZA KUNA SHIDA YA DAWA

Ukanda wa Ghaza, Palestina unakabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa

Ukanda wa Ghaza, Palestina unakabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa

Mkurugenzi Mkuu wa Dawa na Matibabu katika Wizara ya Afya na Tiba ya Palestina amesema kuwa eneo la Ukanda wa Ghaza linakabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa.

Munir al Barish ameeleza kuwa mashambulizi makubwa yanayofanywa dhidi ya Ukanda wa Ghaza yamesababisha uhaba mkubwa wa dawa kiasi kwamba aina 130 za dawa muhimu za matibabu zimemalizika katika eneo hilo lililoathiriwa na vita, ambapo aina 50 kati ya dawa hizo ni zile zinazotumika katika upasuaji.

Watoto wa Kipalestina wa Ukanda wa Ghaza wakiwa chini ya mzingiro wa Israel

Huko nyuma Madhat Muhsein Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Hospitali katika Wizara ya Afya na Tiba ya Palestina alitangaza kuwa Ukanda wa Ghaza unakabiliwa na upungufu wa dawa aina 30 hadi 35, vifaa na suhula za kitiba na maabara huku eneo hilo likihitajia pia wafanayakazi 800 wa sekta hiyo.

Utawala wa Kizayuni uliuzingira Ukanda wa Ghaza tangu mwaka 2006 baada ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas kushinda uchaguzi wa bunge na kisha ukazuia kuingizwa katika eneo hilo dawa, suhula za kitiba na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya wananchi wa Palestina.