Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:56 am

NEWS: IKUPA: 'WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA MVUA KWA SHUGHULI ZA UZALISHAJI'.

DODOMA: Serikali imewataka wananchi kutumia fursa chanya ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini kwaajili ya shughuli za uzalioshaji mali.

Hayo yamesemwaleo mjini hapa na naibu waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Stella Ikupa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya tahadharidhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali na hatuazakuchukua .

Amesema ili kufikia maendeleo chanya ni wajibu wa wananchi kutumia mvua hizi kwa ajili ya kilimo,kuandaa mabwawa na malambo kwa ajili ya kuvuna maji,kupanda mazao yanahitaji maji mengi kama vile mpunga,uzalishaji wa samaki na kuandaa malisho.

‘’Kamati za Usimaminzi wa Maafa kuanzia ngazi ya kijiji/mtaa kutekeleza majukumu yake kwa majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya usimaminzi wa maafa namba saba ya mwaka 2015 na kanuni za usimaminzi wa maafa za mwaka 2017,’’amesema Ikupa.

Aidha Ikupa ameongeza kuwa mvua hizo zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na tayari baadhi ya maeneo yaliyotabiriwa kupata mvua nyingi yameanza kupata madhara mbalimbali zilizosababishwa na mafurikoikiwemo vifo, magonjwa ya milipuko, uharibifu wa mazao masahambani , uharibifu wa mazingira , mali na miundombinu.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ilitoa utabiri wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba mpaka Desemba , 2017 kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua tarehe 4 septemba , 2017 .